Aliyekua gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko anatakiwa kufika katika afisi za DCI Jumatatu ijayo kuandikisha kauli kutokana na matamshi aliyotoa kumhusu katibu mkuu wa mambo ya ndani Karanja Kibicho.

Hii ni kutokana na mkuu wa DCI George Kinoti siku ya Jumanne jioni kutoa mwito kwa aliyekua gavana wa nairobi akimrai kufika katika makao makuu ya DCI Kiambu.

Sonko atahitajika kuangazia madai aliyotoa kumhusu Kibicho kuhusika katika uchafuzi wa jina ya chama cha ODM mnamo mwaka 2017. Sonko alitoa madai hayo akiwa katika mkutano wa kisiasa Dagoretti Kusini.

 Kulingana na Sonko akiwa na Kibicho na watu waliotajwa kama ‘ Deep state’ walipanga njama na kuchoma magari ili kuchafua jina la chama cha ODM.

Aidha kwa upande wake Kibicho amesema kua atafuatilia kesi hiyo kwa kina baada ya Sonko kujaribu kumchafulia jina.

Story by Lavine Wanzetse

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE