Serikali ya kitaifa imetakiwa kuharakisha ujenzi wa barabara kuu ya kutoka Kisumu kuingia mjini Busia ili kurahisisha shughuli za uchukuzi katika eneo hilo la mpakani.

Naibu Gavana wa kaunti ya Busia Moses Mulomi, anasema licha ya serikali ya kitaifa  kunuia kujenga soko kuu la jumuia mpakani Busia, kuna haja ya kuharakishwa kwa ujenzi wa barabara ya Kisumu –Busia ili kutatua changamoto ya msongamano wa magari ya masafa marefu ambayo yamerundikana mpakani Busia na Malaba.

Akizungumza na wanahabari baada ya mkutano uliowaleta pamoja washikadau katika sekta mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na kuongozwa na katibu wa kudumu katika wizara ya jumuia ya Afrika mashariki Dr Kevit Desai, Mulomi aidha amesema kuwa serikali ya kaunti ya Busia imeweka mikakati ya kuondoa msongamano wa magari mpakani humo.

Kwa upande wake Dr Desai amesema wananchi watapewa mafanzo ya kibiashara mbali na mikakati zaidi ili kufanikisha mpango huo wa kiteknolojia.

Story by Hillary Karungani 

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE