Mashirika ya kijamii kaunti ya Bungoma sasa yanakitaka chama cha ODM kumwondoa afisini Katibu Mkuu wa chama hicho Edwin Sifuna, kwa msingi kuwa ameonyesha mienendo ambayo huenda ikaathiri chama hicho.

Kwenye kikao na wanahabari mjini Bungoma, wanaharakati chini ya shirika la kijamii la Center for Good Governance wamekosoa cheche za matusi alizotoa Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna akimtusi Rais wa chama cha mawakili nchini LSK Nelson Havi baada ya kuzuiwa kuingia kwenye mkutano wa chama hicho.

Lumumba Wekesa ambaye ni mwanaharakati kaunti ya Bungoma, amemtaka Sifuna kutekeleza wajibu wake kama Katibu Mkuu wa ODM bila kuingilia utendakazi wa Havi, akimtaja Sifuna kuwa aliyemkosea heshima Nelson Havi.

Usemi wake unerejelewa na Philip Sifuna, akikosoa mazoea ya Sifuna kuwatusi na kuwadharau viongozi wengine hasa kutoka eneo la magharibi, hali anayosema inaenda kinyume na utamaduni wa viongozi wa eneo hilo wanaopenda amani.

Semi hizi zinajiri yapata siku moja baada ya kuibuka malumbano ya maneno kati ya Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna na Rais wa LSK Nelson Havi.

Story  by Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE