Nchi hii leo imejiunga na mataifa mengine ya bara Afrika kuadhimisha siku ya kupambana na ufisadi.

Maadhimisho hayo yanatoa fursa kwa wadau wote wa kupambana na ufisadi kutafakari na kushauriana kuhusu jukumu la jumuiya za kiuchumi za kanda katika kuimarisha ajenda ya kupambana na ufisadi.

Kwa utambuzi wa tisho la ufisadi, tarehe ya leo miaka 18 iliyopita, muungano wa Afrika uliidhinisha mkataba wa kuzuia na kupambana na ufisadi barani Afrika mjini Maputo nchini Msumbiji.

Tangu mwaka wa 2017, mataifa ya kanda hii yameadhimisha tarehe 11 mwezi Julai kama siku ya kupambana na ufisadi barani Afrika.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “ jumuiya za kiuchuimi za kanda ni nguzo muhimu katika utekelezaji mkataba wa muungano wa afrika za kuzuia na kukabiliana na ufisadi”.

Wakati uo huo, tume ya maadili na vita dhidi ya ufisadi humu nchini (EACC) na serikali za mataifa ya Afrika imejiandaa ipasavyo kukabiliana na vsia vya ufisadi.

Tume hiyo inasema kufikia sasa mataifa 44 kati ya 55 ya Afrika yametia saini mkataba wa umoja wa afrika kuhusu kuzuia na kupiga vita ufisadi.

Kulingana na mkataba huo, mataifa yanapaswa kuratibu sheria, mifumo na taasisi za kupambana na ufisadi.

Imekisiwa kwamba bara la Afrika litaendela kusalia nyuma ya mataifa mengine ikiwa hali haitabadilika.

Kulingana na ripoti ya hivi punde ya benki ya dunia kuhusu umaskini duniani, hali ya ufukara itaendelea kukithiri barani afrika ikiwa ufisadi hautakabiliwa ipasavyo katika kipindi cha muongo mmoja ujao.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE