Baadhi ya wabunge wa chama cha ODM katika kaunti ya Kakamega wameapa kwamba watamng’atua mamlakani mwenyekiti wa chama hicho kaunti hiyo ambaye pia ni naibu gavana kwenye serikali ya Kakamega profesa Phillip Kutima kwa madai ya uongozi mbaya.

Wakiongea mjini Kakamega, wakiongozwa na mbunge wa Shinyalu Kizito Mugali na Seneta Mteule Naomi Shiyonga, wamedai kwamba tangu profesa Kutima alipoteuliwa kuwa mwenyekiti wa ODM, umaarufu wa chama hicho umerudi chini kwa kiwango kikubwa.

Kulingana na seneta Naomi Shiyonga, wanataka kufufua chama hicho mashinani na wataanza na kufanya mabadiliko ya uongozi kupitia kwa demokrasia ya kuchagua viongozi wapya mbele ya uchaguzi mkuu mwaka ujao.

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE