Zaidi ya wafanyabiashara wadogo wadogo mia nne katika masoko ya Nalondo na Chwele kaunti ya Bungoma wamenufaika na ufadhili wa pesa kupiga jeki biashara yao chini ya mpango wa Inua Jamii Initiative unaolenga kuwafikia takribani wafanyabiashara elfu kumi katika kaunti ya Bungoma.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo, manaharakati Zachariah Baraza amesema nia yake ni kuwapiga jeki wafanyabiashara wadogo wadogo hasa wakati huu wa janga la korona.

Wakati uo huo amemuomba gavana kaunti ya Bungoma Wycliffe Wangamati kuwaondolea ushuru wafanyabiashara wadogo wadogo kama njia ya kuwapunguzia mzigo.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE