Wakaazi wa mkoa wa magharibi mwa Kenya wametakiwa kumuunga mkono kinara wa chama cha ANC Wycliffe Musalia Mudavadi kwenye uchaguzi mkuu ujao
Ni kauli yake mbunge wa Malava Moses Malulu Injendi akizungumza kwenye mahojiano na kituo cha 102.2 Lubao fm
Malulu amesema Mudavadi anao uwezo wa kulikomboa taifa hili haswa katika swala la kiuchumi akimlinganisha na rais wa tatu wa jamhuri wa Kenya
Malulu pia akiipuzilia mbali misimamo kinzani ambayo amekuwa nayo hapo awali akisema imepitwa na wakati na kwa sasa ni wakati wa kutembea naye Mudavadi
Malulu amewataka viongozi wa Magharibi kuja pamoja na kumuunga mkono Mudavadi na kuondoa tofauti zao za kisiasa ili kujipa nguvu kwenye serikali itakayobuniwa baada ya uchaguzi mkuu ujao
Malulu ametabiri uwezekano wa viongozi tokea Mlima Kenya ambao amesema ikikaribia kwenye uchaguzi mkuu ujao watamuacha Naibu wa Rais William Ruto
Wakati uo huo Malulu ameunga swala la kuwataka viongozi wawe na shahada kwenye uchaguzi mkuu ujao kwa wabunge na kurekebishwa kwa kipengee cha wakilishi wadi na wale wa kike kwenye kaunti
Malulu amewarai wakaazi wa eneo bunge lake la Malava kumpa nafasi nyingine ya kuongoza eneo bunge hilo kwenye uchaguzi mkuu ujao ili kuendeleza ajenda alizo kuwa nazo ikiwemo swala la elimu
By Javan Sajida