Viongozi wa kisiasa kwenye kaunti ya Bungoma wamehimizwa kujitenga na matamshi ambayo huenda yakachochea kuwepo vurugu miongoni mwa wananchi.

Mwanaharakati wa kisiasa kaunti ya Bungoma Derick Wafula anasema ubabe wa kisiasa ambao unaendelea kushuhudiwa miongoni mwa wanasiasa kaunti hii huenda ukachochea kuwepo rabsha mbele ya uchaguzi mkuu ujao.

Aidha Wafula amedokeza kuwa licha ya kuibuka madai ya kuwepo sakata mbalimbali zinazowakumba wanasiasa  ambao wameonyesha nia ya kuwania kiti cha ugavana kaunti hii, ni mwananchi aliye na uwezo wa kumchagua atakayeongoza kaunti hii kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Amevitaka vyombo vya usalama kuwatia mbaroni  wanasiasa wanaodaiwa kuchochea vurungu hasa kwenye hafla mbalimbai za mazishi.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE