Kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi ameitaka tume ya IEBC kuwa macho zaidi na makamishna ambao watakapo pokezwa nafasi ya kusimamia tume hiyo 

Musalia amesema lazima makamishna hao wawe watu wenye maadili mema na wamakinike ili wasimamizi wa uchaguzi wasilitoze taifa kwenye tatizo wakati huo utakapofika. 

Mudavadi akizungumza katika kanisa la SDA Mathare Kazkazini kaunti ya Nairobi amesema kuwa kuna umuhimu wa wakenya kuwa macho kuona ni wakenya wagani wanapewa uongozi katika taasisi mbali mbali na hata kwenye nyadhifa za uongozi wa kisiasa kwani kuna viongozi ambao huenda wanasubiri kupokezwa mamlaka na walitumbukize taifa pabaya.

By Javan Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE