Wakulima kutoka kaunti ya Kakamega na nchi kwa jumla wametakiwa kukumbatia teknologia mpya kwenye kilimio cha ufugaji wa nyuki ili kuboresha kiwango cha uzalishaji asali na kuziba pengo la uhaba wa asali humu nchini
Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika moja la humu nnchini linalojihusisha na mradi wa ufugaji wa nyuki Andrew Egala
Egala amesikitikia hatua ya Nchi ya Kenya kuagiza asali kutoka kwa mataifa jirani ilhali kaunti za humu nnchini ikiwemo ya Kakamega yenye mazingara bora ya kuzalisha asali ya kutosha zikikosa kutumia firsa hiyo. akisokeza kuwa wakati umewadia wa kukumbatia mbinu mpya za kilimo hicho ilikufaidika nacho
Naye mkurugenzi wa kiuo cha utafiti cha kilimo kaunti ya Kakamega Joseph Munyasi akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa aina mpya ya mizinga ya nyuki amesema kua tatizo kuu la ukoseph wa mizinga ya kisasa ambalo lilikuwa likiwakumba wakulima hao huenda likafika kikoma kwa uzinduzi mpya wa mizinga hiyo na hata kuimarisha kilimo hicho cha nyuki
By Richard Milimu