Huku wanafunzi wakiendelea kuripoti shuleni baada ya kusalia nyumbani kwa muda mrefu kufwatia kuzuka maambukizi ya virusi vya corona, swala la uhaba wa miundo msingi shuleni limetajwa kama changamoto kuu na lapaswa kushughulikiwa upesi.

Akizungumza afisi mwake mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wavulana ya teremi eneobunge la kabuchai benard wamanga amesema licha ya wanafunzi kurejelea masomo yao bado wanakumbwa na changamoto ya miundo msingi japo amedokeza kuwa mikakati imewekwa kufwatia swala hilo.

Wakati uo huo wamanga amedokeza kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi wamewasili shuleni huku akihoji kuwa  huenda changamoto ya fedha na usafiri imechangia baadhi yao kutorejea shuleni kwa wakati unaofaa.

Amewataka wazazi kuhakikisha wanafunzi wanaripoti shuleni huku wakiendelea kushughulikia karo yao.

by richard milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE