Wito umetolewa kwa serikali ya kaunti ya bungoma kuingilia kati na kuwatafutia soko wakulima wa kahawa kama njia mojwepo itakayowawezesha kupokea malipo bora yatakayofanikisha miradi yao mbalimbali.

Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha kapkrong wadi ya chesikaki eneobunge la mlima elgon stephen ndiwa  akizungumza wakati wa kuongoza hafla ya kutoa malipo kwa wakulima wa chama hicho, anasema kilimo cha kahawa kitawafaidi wakulima iwapo serikali ya kaunti hii itafanya juhudi za kuwatafutia soko katika mataifa ya kigeni.

Wakati uo huo ndiwa amedokeza kuwa licha ya kupokea kahawa kwa kiwango cha chini msimu uliopita bei ya zao hilo iliimarika pakubwa.

Naye mkurugenzi katika chama hicho cha kapkrong edward wasike akiwataka wazazi kuwatengea wanao ardhi ya kupanda kahawa semi zilizoungwa mkono na bi violet khanjila.

BY Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE