Familia moja kutoka mtaa wa mlimani eneo bunge  la likuyani kaunti ya kakamega imejitokeza wazi na kuomba msaada wa kugharamia matibabu ya mwanao ambaye kwa hivi sasa bado amelazwa katika hospitali ya cherengany nursing home kaunti ya trans nzoia…

Kwenye mkao na kituo hiki , mamake ben kimani kibet  bi. Josephine kipkosigei,alisimulia kuwa mwanawe alipigia na jamaa mmoja ambaye yuko mafichoni hadi wa leo  , na kwa hivi sasa mwanawe anaendelea kuuguza majera katika hospitali ya cherengany nursing home kwa muda wa miezi mitatu  sasa, huku   gharama ya matibabu ikiendelea kupanda.

Aidha bi. Josephine kipkosigei  ameomba wasamaria wema kujitokeza na kumsadia gharama ya matibabu ya mwanawe  ambaye kwa hivi sasa anadaiwa zaidi ya kima cha takribani  shilingi elfu mia nane , na bado kijana huyo hajapata nafuu

Kauli hiyo iliungwa mkono na nyanyake jamaa huyo mary wanjiru ,ambaye alihoji kuwa kutokana na hali yake ya uchochole hatamudu gharama ya matibabu ya  mjuguu wake

Mike omore jiraniye familia hiyo ametoa wito kwa wahisani kusaidia familia hiyo , ikizingatiwa kuwa mapato yao ni madogo  mno  , huku nyanyake akiwa ni muuza mboga kwa kibanda ambayo haizi gharamia matibabu yake ben

Story by Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE