Watoto wa kurandaranda mitaani mjini kakamega sasa wanataka mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yamekuwa yakituma maombi ya misaada katika mataifa ya ughaibuni kwa niaba yao, kuchunguzwa kwa madai ya ufisadi na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Wakizungumza na kituo hiki baada ya kuhudhuria mazishi ya mmoja wao wilfred kamau mwenye umri wa miaka 16 katika eneo bunge la shinyalu, watoto hao wa kurandaranda wamesema inasikitisha kuona wao wakiendelea kutaabika na kulala kwenye baridi kila siku, ilhali kuna watu wachache wanaonufaika kutokana na ufukara wao.
Vijana hao wameitaka serikali ya kaunti hiyo kutenga fedha za kuwasaidia watoto mayatima kama njia mojawapo ya kupunguza watoto wa kurandaranda mijini.
Wakati uo huo, pastor wa kanisa la full gospel duncan omondi, amewataka wazazi kuwajibikia malezi ya wanao ili kuwazuia kuanza kujiunga na vikundi vya kurandaranda mitaani.
BY RICHARD MILIMU