Gavana Ottichilo aidha ameelezea kwamba fomu za kufadhili masomo kwenye shule na vyuo mbalimbali maarufu kama bursary  zipo tayari  na kuwataka wanaohitaji fedha hizo kuzichukua fomu kwenye ofisi za wodi.  

Hata hivyo Ottichilo ameelezea hatua ambazo serikali yake imepiga kwenye idara ya chekechea ikiwemo ujenzi wa madarasa 175 ya chekechea na mengine 30 yatakayojengwa kwenye mwaka huu wa kifedha.  

Wakati uohuo afisa mkuu wa chekechea Dkt. Mary Anyienda ameelezea kwamba vifaa vilivyo tolewa leo ikiwemo sabuni, mitungi ya kunawia mikono,  barakoa,  viti na meza  vinanuiwa kumsaidia mwalimu na wanafunzi wa chekechea kufuata sheria za udhibiti wa covid 19. 

Vile vile anyienda amewasihi waalimu walioajiriwa na serikali ya kaunti mwaka jana kudumisha uhusiano mwema na viongozi wa shule wanakofunza.  

Hata hivyo,  Anyienda amewaelezea waalimu ambao marupurupu yao hayajalipwa kwa muda kuwa na subira huku akiwahakikishia kuwa marupurupu hayo yatalipwa ifikapo mwishoni mwa mwezi wa Januari.

by Lillian Mmbone

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE