Hali ya taharuki imetanda sokoni Makunga wilayani Navakholo baada ya mtu mmoja anayeshukiwa kuwa jambazi kupigwa risasi na kuwawa na polisi huku mmoja akitoroka na majeraha ya risasi usiku wa kuamkia leo
Polisi wanasema kuwa wawili hao walikuwa miongoni mwa genge la wezi walokuwa wakijaribu kutekeleza wizi kwenye hoteli moja maarufu eneo hilo (Lantana comfy)
Wakaazi kwa upande wao wamewapongeza polisi kwa tukio hilo baada ya visa vya wizi kuonekana kukithiri
“Maaskari wa makunga tunasema asante kwa sababu kazi mmefanya ni mzuri sana. Kando na hoteli na vilabu bado wezi wanaweza kuja kwa boma zetu,”
Akizungumza eneo la tukio mwakilishiwadi wa Makunga Isongo Malaha eneobunge la Mumias Mashariki Lucas Radoli ametaka kuwepo na ushirikiano kati ya maafisa wa polisi wa Navakholo na wale wa Mumias Mashariki kuimarisha usalama eneo hilo
“Afisa wa usalama Upande wa mumias East mushirikiane na afisa wa usalama wa Makunga na kuwe na usalama. si vizuri raia kuweka sharia mikononi mwao kwa hivyo askari wakishirikiana itakua vyema na usalama utaimarika.”
Vyongozi wengine walokashifu hali duni ya usalama ni mwanasiasa Johnathan Chacha aliyetaka pawepo na kituo kidogo Cha polisi sokoni humo
Chacha vile vile amewaonya vijana wanaohusika na visa vya kihalifu sokoni Makunga na kuwataka maafisa wa usalama kuwachukulia hatua mwafaka
“Vijana wetu lazima wapate kazi ya kufanya na waachane na uhalifu. Si vyema kuhatarisha maisha yako kama kijana kwa kujiunga na vikundi vya uhalifu na pia kuhatarisha maisha ya raiya wengine. Ningeomba polisi wakati mnakutana na vijana waalifu musiwaurumie malizana nao hapo hapo kwamaana wamekua tisho kwa wenyeji”
Mmojawapo wa waathiriwa wa vitendo vya kihalifu mwanasiasa Stephen Makokha amewasuta wakuu wa polisi kwa utepetevu
“Afisa wa polisi kwa mara mingi wanatajwa kushirikiana na wahalifu. Nawalaumu wakuu wa polisi kwa maana hawafanyi uchunguzi wao na wakati visa vinapotokea na kuripotiwa washukiwa hutaja afisa wa polisi kwa ushirikiano.”
Mwanasiasa huyo aliibiwa bidhaa pamoja na kiwango Cha pesa kisichojulikana siku mbili zilizopita katika duka lake la vinywaji huu ukiwa ni msururu wa visa vya wizi hiki kikiwa Cha 6 kwa mwezi huu pekee sokoni Makunga
Story by James Nadwa