Muungano wa wakulima wa samaki Walukak Fish Farming umekutana leo katika kaunti ya Kakamega kata ndodo ya Malava kata ya Kabras Kusini eneo la Shianda kijiji cha Muluanda ambapo lipo  bwawa wanalolitumia kufuga samaki wao.


Akizungumza kwenye mkutano huo Tom Oremo ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho alisema walikuwa wamekusanyika hapo ili kuchukua sampuli ya samaki na kupeleka kwenye kiwanda cha samaki kwa minajili ya kukaguliwa, aliendelea na kusema changamoto zinazo wakabili kama wafugaji wa samaki na pia kuomba msaada kutoka kwa serikali ili kuendeleza vyema mradi huo


Tom alishukuru shirika la Kenya Climate Smart Agriculture kwa kuwashika mkono na pia mkurugenzi mkuu wa Lubao FM bwana Charles Oduor kwa kuwasaidia kimawazo na pia kwa kua mwanachama

Naye Hellen Abwao amabaye ni katibu wa chama hicho alisema kuwa  walianza chama hicho wakiwa wadhaifu lakini baada ya kuungana na shirika la Kenya Climate Smart Agriculture kaunti ya Kakamega waliweza kufikia malengo yao

kwa upande mwingine Samuel Adek ambaye ni mweka hazina wa chama hicho alieleza jinsi wizara ya hazina katika chama hicho ipo katika mstari wa mbele kuhakikisha kuwa Lukak fish farming inafanikisha miradi yake bila tashwishi

Naye Moses Kigen, mwakilishi wa miradi ya kata alisema kuwa wanachama wa Lukak wako na bidii kwani wameweza kusaidika na mradi huo mingahiri ya changamoto wanazopitia

Naye miriam chepkania kutoka shirika la Kenya Climate Smart Agriculture alieleza malengo ya shirika lake kwa wanachama wote wanaofadhiliwa na shirika hilo haswa sana muungano wa Lukak fish farming

Martin Otieno ambaye ni muhandisi wa Lukak fish farming alieleza jinsi shirika la benki ya duniani ilivyo ungana na yeye ili kuwezesha mradi wa kufuga samaki na pia kueleza alivyo tengeneza bwawa hilo

Nao wanachama walieleza changamoto walizokuwa wamepitia hapo awali kabla ya kupata msaada kutoka kwa shirika la Kenya Smart Agriculture
By Winny Akinyi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE