Wakulima wa zao la pamba kutoka eneobunge la Sirisia wamehimizwa kujiandikisha katika afisi husika ili kupokea mbaegu itakayosaidia kuzidisha mapato kwenye kilimo hicho.

Akizungumza baada ya kuongoza zoezi la kuwapiga msasa wawaniaji viti mbalimbali katika chama cha ushirika cha Namang’ofulo eneobunge la Sirisia, mkurugenzi wa vyama vya ushirika eneo hilo Pius Mbai amedokeza kuwa hivi karibuni watawakabidhi wakulima mbegu ya pamba na kuwataka kutilia maanani kilimo hicho.

Wakati uo huo Mbai amewataka wawaniaji viti mbalimbali kuhakikisha wanadumisha amani wakati wa  zoezi la uchaguzi ambalo linatarajiwa kuandaliwa alhamisi juma hili.

Ni matamshi yalioungwa mkono na mwenyekiti wa chama cha ushirika cha Namang’ofulo Patrick Simiyu Barasa.

Aidha Simiyu ametoa wito kwa mbunge wa eneo hilo John Waluke kuunganisha nguvu za umeme kwenye chama hicho ili kurahisisha shughuli mbalimbali.

By Hillary Kaungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE