Chifu wa kata ndogo ya Makunga wilayani Mumias Mashariki Willy Rapando amelalamikia ongezeko la wizi wa ngo’mbe eneo hilo siku  za hivi punde

Akiongea kwenye hafla moja ya mazishi mtaa wa Ikoli eneobunge hilo Rapando amehoji kuwa wingi wa visa hivi hutokea nyakati za usiku na kutoa onyo kali kwa wahusika kuwa watakumbana na mkondo wa sheria

Kauli hiyo iliungwa mkono na mbunge wa Mumias Mashariki Ben Washiali aliyevitaka vitengo vya usalama kumakinika na kuwahakikishia wakaazi usalama wao

Washiali aidha amesema kuwa wamo mbioni kumalizia vituo kadhaa vya polisi kikiwemo cha Isongo na kile cha Mutono ili kuimarisha usalama

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE