Ni usemi wake mshauri wa serikali hiyo ya kaunti kwa maswala ya uongozi ali Musa Chibole
Kwenye mahojiano ya kipekee na idhaa hii Chibole amesema kuwa serikali ya kaunti ya Kakamega huwalipia karo watoto werevu kutoka jamii zisizo jiweza kama njia mojawapo ya kufanikisha masomo yao
Chibole hata hivyo amelaumu uhamisho wa walimu hadi sehemu tofauti kama baadhi ya visababishi vya kudorora kwa viwango vya masomo kwenye kaunti hiyo
Kuhusu hali ya uhaba wa dawa kwenye baadhi ya hospitali eneo la magharibi Chibole amewasuta baadhi ya wafanyikazi kwenye idara ya afya tatizo hilo akiapa kuchukua hatua zifaazo
Haya yanajiri huku tatizo la uhaba wa dawa likizidi kushuhudiwa kwenye vituo kadhaa vya kiafya kikiwemo cha shianda na kile cha makunga eneobunge la Mumias Mashariki
By James Nadwa