Ni afueni kwa wakulima wa samaki kutoka kaunti zilizoko kwenye muungano wa kiuchumi wa ziwa baada ya kiwanda cha kuhifadhi samaki kuzinduliwa katika kaunti ya kakamega kama njia moja ya kupiga jeki uchumi wa eneo hilo pamoja na kutatua changamoto zinazowakumba wakulima wa samaki
Akizungumza kwenye hafla kuzindua kiwanda hicho katika eneo la lutonyi eneo bunge la lurambi, gavana wa kaunti ya kakamega ambaye pia ni mwenyekiti wa muungano huo wycliffee oparanya amesema kiwanda hicho kitasaidia pakubwa katika kuboresha uchumi wa eneo hili huku akidokeza kuwa serikali yake imeweka mikakati maalumu ya kusaidia kilimo cha samaki katika kaunti ya kakamega
Oparanya aidha amesema kuna haja ya kaunti husika kushirikiana ili kuhakikisha ufanisi wa eneo zima la ziwa, usemi ulioungwa mkono na naibu mwenyekiti wa ukanda huo ambaye pia ni gavana wa kisii james ongwae ambaye amesema utendakazi wa kiwanda hicho utazuia samaki kusafirishwa kutoka maeneo mengine jambo linalowanyima wakulima wa eneo hilo soko…………….
aidha balozi wa taifa la uswidi nchini kenya bi caroline vicini amesema taifa la uswidi liko tayari kushirikiana na taifa la kenya katika mradi huu wa samaki kuona wakulima wanafaidika huku akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa uwazi katika mchakato huo mzima
Kwa upande wake waziri wa ugatuzi eugine wamalwa aliyehudhuria hafla hiyo amewataka wakazi wa ukanda huu kuangazia aina kadhaa za kilimo kando na miwa na mahindi huku akiwataka wanasiasa kutoka maeneo haya kusita kupiga siasa potovu zinazowaogopesha wawekezaji kuekeza
By Linda Adhiambo