Ni  afueni  kwa  wakulima  wa  samaki  kutoka   kaunti   zilizoko  kwenye  muungano wa kiuchumi wa ziwa baada ya kiwanda  cha kuhifadhi samaki  kuzinduliwa  katika  kaunti  ya  kakamega  kama  njia  moja  ya  kupiga  jeki  uchumi  wa  eneo hilo pamoja na   kutatua changamoto zinazowakumba wakulima  wa  samaki

Akizungumza  kwenye  hafla  kuzindua  kiwanda hicho  katika eneo la  lutonyi   eneo bunge la lurambi, gavana  wa  kaunti  ya  kakamega  ambaye  pia  ni   mwenyekiti  wa  muungano huo wycliffee  oparanya   amesema kiwanda hicho  kitasaidia  pakubwa katika  kuboresha  uchumi  wa  eneo hili huku akidokeza kuwa  serikali  yake  imeweka mikakati  maalumu  ya  kusaidia  kilimo   cha  samaki katika kaunti  ya  kakamega  

Oparanya  aidha amesema  kuna haja ya kaunti husika kushirikiana ili kuhakikisha ufanisi wa eneo zima la ziwa,  usemi  ulioungwa  mkono  na  naibu  mwenyekiti  wa   ukanda  huo  ambaye  pia  ni  gavana  wa  kisii  james  ongwae ambaye amesema utendakazi wa kiwanda hicho utazuia samaki   kusafirishwa kutoka  maeneo mengine jambo linalowanyima  wakulima wa eneo hilo soko…………….

 aidha balozi  wa  taifa  la  uswidi  nchini  kenya  bi  caroline  vicini amesema  taifa  la  uswidi  liko  tayari  kushirikiana  na  taifa  la  kenya  katika  mradi huu  wa  samaki kuona wakulima wanafaidika huku akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa uwazi katika mchakato  huo mzima  

Kwa upande wake waziri  wa ugatuzi  eugine  wamalwa  aliyehudhuria hafla  hiyo  amewataka  wakazi  wa  ukanda huu  kuangazia  aina kadhaa za kilimo  kando na miwa na mahindi huku akiwataka wanasiasa kutoka maeneo haya kusita  kupiga siasa  potovu zinazowaogopesha wawekezaji  kuekeza

By Linda Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE