Ni afueni kwa wakaazi ambao ni wafugaji na wanunuzi wa samaki kwa kaunti 14 za muungano wa Lake Region Economic Block LREB ikiwemo kaunti za mkoa wa Nyanza na Magharibi mwa Kenya baada ya kufunguliwa rasmi kiwanda kitakacho fanikisha mauzo ya samaki katika eneo la Lutonyi eneo bunge la Lurhambi kaunti ya Kakamega 

Gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya amesema mradi huo umeigharimu serikali ya kaunti ya Kakamega shilingi milioni 20 huku serikali kuu ya kitaifa ikisaidia kwa kuwapa shilingi milioni sita nalo shirika la kibinafsi la DOS Group Kenya LTD likiwekeza kitita cha shilingi milioni 40 ili kuwezesha kiwanda hicho kilichoanzishwa mwaka 2009 kufikia hali ya kuruhusu kuendelea kwa mauzo ya samaki 

Hata hivyo gavana Oparanya amesema kando na kilimo cha miwa na mahindi ambacho kimekuwa kikikuzwa eneo hili serikali yake ilionolea kuanzisha kiwanda hicho baada ya ufugaji wa samaki kuongezeka na pia kuongezeka kwa soko la samaki 

Naye gavana wa kaunti ya kisii ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la magavana nchini aliyehudhuria hafla hiyo amesema kuanzishwa kwa kiwanda hicho kutawafaidi wafugaji wa samaki toka eneo pana la ziwa wala si kaunti ya Kakamega pekee akisema zao hilo litamaliza uaguzaji wa samaki kutoka uchina akisema anatarajia usaidizi kutoka kwa serikali ya uswizi

Naye waziri wa ugatuzi nchini Eugine Wamalwa ambaye alikuwa kwenye mkao huo amewataka wanasiasa toka magharibi mwa Kenya kuchunga ndimi zao na matamshi ya kisiasa amvayo huwenda yasiwavutie waekezaji zadi kujitokeza na kuwekeza magharibi mwa kenya na kudidimiza ufufuzi wa viwanda vikiwemo vya miwa huku akishabikia mradi wa ufugaji wa samaki 

Naye balozi wa Uswizi nchini Caroline Vicini ambaye alikuwa mgeni mashuhuri kwenye sherehe hizo amesema serikali ya Uswizi itaendelea kupiga jeki ukuwaji wa soko la samaki nchini akitaraji mradi huo utafaidi wakulima wengi nchini pamoja na makundi ya kina mama na vijana

By Javan Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE