Muungano wa KUPPET kaunti ya Kakamega umeondoa walimu lawamani kuhusu swala la dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi
Akiongea kwenye hafla ya kuchangisha pesa kusaidia mazishi ya mwalimu mmoja eneo la Ahisiru Lurambi mwenyekiti Johnston Wabuti amesema walimu hawapasi kuhusishwa na lawama kwani ni jukumu la serikali
Wabuti kwa upande mwingine amelalamikia idadi ndogo ya nafasi za kuajiri walimu akiitaka tume ya TSC kuongeza kiwango
Vile vile ametaka swala la mwaka wa kumaliza chuo kuzingatiwa katika zoezi la kuajiri walimu
By Lindah Adhiambo