Baadhi ya wawaniaji viti vya kisiasa katika chama cha ODM kaunti ya Kakamega wameunga mkono pendekezo la afisi kuu la kupeana tiketi ya moja kwa moja kwa wawaniaji ambao wataonekana kuwa na nguvu
Wakiongea mjini Kakamega kupitia kwa Habil Nanjendo wa Butere wamesema chama cha ODM kilipoteza viti kwa sababu ya baadhi ya wanasiasa walegevu kutumia mchujo kujipatia tiketi
Hisia zao zimetikana na mkutano wa mwishoni mwa juma ulioongozwa na gavana Wycliffe Oparanya na katibu Edwin Sifuna na wametaka juhudi za kurekebisha afisi ya kaunti kuharakishwa ili kuthibiti chama
Nanjendo pia ameunga mkono muungano wa ODM na Jubilee akisema kama ODM walichezwa shere na muungano wa NASA
By Lindah Adhiambo