Vyongozi wa kisiasa pamoja na wakulima kadhaa kutoka eneobunge Navakholo wamefanya ziara ya ghafla kwenye kiwanda Cha sukari Cha Mumias kutaka kutathmin hali ilivyo kwenye kiwanda hicho

Wakiongozwa na mwakilishiwadi wa Shinoyi Shikomari Esumeeya eneobunge la Navakholo Bonface Akosi pamoja na mwanaharakati wa kisiasa Dan Mustotso Mmayi vyongozi hao wamefdheheshwa na hali ilivyo huku wakiwasuta wasimamizi wa kiwanda kwa kutokuwa na nia ya kukifufua kiwanda hicho

Aidha wamemlaumu mrasimu kwa kukosa kuweka mikakakti bora ya kunisaidia kampuni hiyo ambayo kwa sasa inayumba

Vyongozi hao vilevile wamewaonya matapeli pamoja jamii zinazoishi sehehu hizo kama kizingiti kwa juhudi za kufufua kiwanda hicho

Wakulima waloandamana na vyongozi hao wakiongozwa na Ben Shibona wametaka pawepo na ushirikiano baina ya wasimamizi wa kiwanda hicho ili kukiwezesha ku rejelea shuguli zake

Haya yanajiri huku baadhi ya wakulima na wakaazi kwenye maeneo yanayokizunguka kiwanda Cha Mumias wanidaiwa wakivamia baadhi ya Mashamba na kuendeleza ukulima wa mahindi huku baadhi ya mali ya kampuni hiyo ikiwemo vyuma na mitambo  ikiuziwa madalali na matapeli licha ya kampuni kuwa chini ya mrasimu

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE