Huku ligi ya Kenya ikitarajiwa kurejea hivi karibuni Hapo Jana Manchester united na Villarreal walijikatia tiketi ya kuingia fainali ya kombe la Europa baada ya kuwabandua Roma na Arsenal mtawalia, Roma walipigwa jumla ya mabao 8-5 huku Arsenal wakilabuliwa 2-1
Tukisonga mbele ni kwamba Liverpool wamekubaliana kuhusu masharti binafsi na kiungo wa kati wa Ufaransa na RB Leipzig Ibrahima Konate mwenye umri wa miaka 21, anayejiandaa kujiunga na klabu ya primia kwa mkataba wa miaka mitano
Hayo yakijiri West Ham imejiunga na Chelsea na vilabu vingine katika mbio za kumnasa mshambuliaji wa Brentford Ivan Toney mwenye umri wa miaka 25, ambaye ana gharama ya pauni milioni 35.
Tukisalia Liverpool Mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah anataka kuondoka Liverpool na Paris St-Germain wanapanga kumpata mchezaji huyo mwenye umri wa miaka28, ikiwa mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe ataondoka majira ya joto
By Samson Nyongesa