Hatimaye wanachama  wa muungano wa kutetea maslahi ya walimu nchini KNUT tawi la Bungoma Magharibi wameshiriki zoezi la kuwachagua viongozi wao watakaosimamia ustawi wao(teachers welfare) huku viongozi hao wakitakiwa kuwa waadilifu.

Akihutubu baada ya zoezi hilo lililoandaliwa katika shule ya msingi ya Busakala eneobunge la Kabuchai katibu mkuu wa muungano wa KNUT tawi la Bungoma Magharibi Moses Masika, amedokeza kuwa uchaguzi huo uliendeshwa kwa njia huru na haki na akiwataka viongozi hao kuwahudumia walimu pasi na upendeleo.

Kwa upande wake naibu katibu mkuu wa KNUT tawi hilo Geofrey Kutu akiwataka walimu kupokea chanjo dhidi ya virusivya corona, huku mwenyekiti aliyechaguliwa kusimamia maslahi ya walimu hao Isaac Wafula akiahidi kuchapa kazi kwa bidii.

Na kufwatia madai ya kuwepo usimamizi mbovu wa basi la walimu hao, Gilbert Kisiombe ameahidi kurejesha usimamizi bora kwenye sekta hiyo muhimu ili kuwafaidi walimu wote.

By Richard Milimu 

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE