Baba askofu jimbo katoliki la Kakamega na pia msimamizi wa jimbo katoliki la bungoma Joseph Obanyi Sagwe, ambaye pia ni mwenyekiti wa tume  ya mawasiliano ya kijamii ya mkutano wa maaskofu wakatolilki nchini Kenya aliweza kuwaongoza wanahabari pamoja na washikadau wa mawasiliano katika  jimbo kwenye misa Takatifu ili kuadhimisha sherehe za hamsini na tano ya mawasiliano ulimwengu mzima. Katika ujumbe wake, aliweza kuwapongeza wana mawasiliano kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwahakikishia kwamba watazidi kuekwa  kwenye maombi

Hata hivyo, aliweza kuwatahadharisha wanahabari dhidhi ya kusambaza habari zisizo za ukweli na zenye propaganda kwani zitachangia katika uhasama kwa maisha ya binadamu

Wanahabari mulioko apa tuweze kusema ukweli na kile ambacho tumekiona. acha wote tufate usemi wa {come and see} ili tupeane ujumbe wa kweli ulimwenguni.

Aidha, alitambua baadhi ya changamoto ambazo wana mawasiliano hupitia ili kuzileta habari hizo pembeni. Akiangazia maswala ya ugonjwa wa covid-19 aliwasifia wanahabari kwa kujituma kwao bila kujali hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo

wanahabari tunawapongeza muliweza kuhatarisha maisha yenu ili kuhakikisha kuwa tunapata habari kuhusiana na ugojwa wa corona na vile vile muliweza kuingia katika mazingara ambayo ni ya kuhatarisha kabisa na nasema pongezi kwenyu

Vilevile, askofu Obanyi alisikitikia visa vya ufisadi na kutowajibika katika taifa la Kenya kufuatia ripoti za hivi maajuzi kwamba dawa za kupunguza ukali wa virusi vya ukimwi (arvs) zimechelewa kufika kwenye hospitali zaidi ya wiki mbili huku zikileta hali ya taharuki kati ya wale wanaoishi na virusi hivyo.

Hafla hio ilihudhuriwa na afisi ya mawasiliano jimbo katoliki la Nakuru likiwakilishwa naye mtawa Micchelle Njeri, wanahabari kaunti ya Kakamega na wana mawasiliano katika jimbo katoliki la Kakamega.

By Tomcliff Makanga And Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE