Familia ambazo nyumba zao zilibomolewa wiki jana kutokana na mzozo wa ardhi katika kijiji cha Nanyeni eneo bunge la Matungu kaunti ya Kakamega na kwa sasa baadhi yao wanaishi  nje ya msikiti  wanadai kupitia kwenye changamoto nyingi zikiwemo za kukosa mahitaji muhimu ya kimsingi yakiwemo maji , chakula na malazi huku wakiitaka serikali kuingilia kati kuwasaidia

Wakiongozwa na Mwanaisha Sena ajuza wa miaka sabini wanasema kuwa kwa sasa wengi wao wanakesha kwenye kijibaridi , kukosa chakula na maji pamoja na malazi baada ya kupoteza kila kitu kwenye ubomozi wa nyumba zao 

Wakatii huo wamelalamikia kubomolewa kwa madrasa ambapo watoto wao walikuwa wakisomea somo la kidini huku wakiitaka serikali kuingilia kati kuzuia maafa ya kukosa maji safi na kijibaridi haswa kwa watoto

Kwa upande wake Mohammed Munyendo ambaye ni mmoja wa waasiriwa amekashfu kitendo hicho akisema kuwa wako na stakabadhi zote za shamba hilo linalozozaniwa akisema waliliridhi kutoka kwa mababu zao.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE