Viongozi mbalimali kautoka kaunti ya Kakamega wameendelea kukashfu mauwaji yaliyotekelezwa katika shule ya upili ya wavulana ya Kivaywa ambayo yalipelekea mabawabu wanne kupoteza maisha yao.

Wa hivi ni naibu gavana wa Kaunti ya Kakamega prof.Philip Kutima ambaye alizuru shule hiyo akiwa ameandamana na viongozi wa kaunti hiyo ambapo amelaani vikali mauwaji hayo huku akiwataka walimu, wazazi pamoja na wanafunzi wa shule hiyo kuwa watulivu huku polisi wakiendelea na uchunguzi.

Kwa upande wake mwanaharakati wa kisiasa Nabii Nabwera ameelezea kusikitishwa kwake na hali ya usalama shuleni humo vilevile akiwataka wenyeji wa eneo hilo kuwa watulivu uchunguzi ukiendelea ili kuwanasa waliohusika na mauwaji hayo.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE