Hali ya huzuni imetanda katika shule ya upili ya wavulana ya Kivaywa iliyoko eneo bunge la Lugari kaunti ya Kakamega baada ya mabawabu wanne kuuawa na genge la watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo Tom Shavisa ni kuwa genge la watu wasiojulikana lilivamia shule hiyo usiku wa manane na kuwaua wanne hao kabla ya kutoweka na vifaa kadhaa vya kielektroniki vyenye dhamana ya maelfu ya pesa.

Kwa upande wao wakaazi wanaoishi karibu na shule hiyo wakiulaumu usimamizi wa shule hiyo kwa kukosa kuweka mikakati ya kutosha ya kuthibiti hali ya usalama shuleni  humo.

Ni kisa kilichothibitishwa naye kamishna wa kaunti ya Kakamega Pauline Dola ambaye amewataka wananchi kujitokeza na kutoa habari muhimu itakayosaidia kuwatia mbaroni washukiwa wa mauwaji hayo.

By Javan Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE