Vyongozi mbalimbali wanazidi kutoa hisia zao kuhusu masharti mapya alotangaza rais kama njia mojawapo ya kukabili msambao wa virusi vya Corona
Afisa msimamizi wa maswala ya jinsia na watoto kaunti ya Kakamega Peninah Mukabane amewataka wanasiasa kutoingiza siasa kwenye swala hilo
Mukabane amekanusha masharti hayo kuulenga mrengo wowote wa kisiasa na kuwataka Wakenya wote kuyakumbatia
Afisa hiyo hata hivyo amewatahadharisha polisi dhidi ya kutumia nguvu kupita kiasi jinsi ilivoshohudiwa hapo awali
Hata hivyo Mukabane amewataka walimu kutowabagua watahiniwa haswa watakaopatikana na ujauzito wakati huu wanapojiandaa kwa mtihani wao wa kitaifa
Haya yanajiri huku zaidi ya watahiniwa milioni4 wakitarajiwa kuukalia mtiani wa kitaifa kote nchini baadaye wiki hii