Mwanaume mwenye umri wa miaka 45 kwa majina Andrew Soita Webo kutoka kijiji cha Luichi kata ya Chegulo eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega ameteketezwa na wananchi wenye hamaki na kufariki baada ya kupatikana akiwa amemjinja ng’ombe ambaye alikuwa ameibwa kutoka boma moja sehemu hiyo.
Wakizungumza na kituo hiki wakaazi wa eneo hilo wakiongozwa na mzee wa mtaa Charles Webo wamehoji kuwa mwanaume huyo alimchinja ng’ombe huyo ndani ya nyumba yake jambo ambalo limewaacha vinywa wazi kabla ya kumtekeketeza.
Akithibitisha kisa hiki chifu wa eneo hilo Juma Inzai amehoji kuwa mabaki ya mwili wa mwenda zake yamepelekwa kwatika chumba la kuifadhi wafu cha hosipitali ya Webuye.
Hata hivyo Inzai amelaani kitendo hicho na kuwaonya wananchi dhidi ya kujichukulia sheria mkononi mwao.