Timu za Mung’ang’a FC na Eshialhulo FC kutoka wadi za East Wanga na Malaha/Makunga/Isongo ndizo zitakazowakilisha eneobunge la Mumias Mashariki katika mashindano ya Oparanya Cup mwaka huu wa 2021.

Timu ya Eshialhulo FC iliweza kufusu katika mashindano hayo baada ya kuwaondoa mababe wa soka Makunga Scopion katika maondoano na hapo jana kutoka sare ya kutofungana naShianda FC kabla ya kuwalambaza magoli mawili Ombwe Lusheya FC mitanange iliyogarakazwa katika uwanja wa Bumini. Mung’ang’a FC ilijikatia tiketi baada ya kuchukuwa alama tatu za bure kutoka kwa Ekero FC iliyodinda kufika uwanjani na baadaye kuwanyuka wana Isongo FC goli moja komboa ufe mitanange liyoandaliwa katika chuo cha mafunzo cha utabibu cha Shianda(KMTC)

Kwa upande wake mkufunzi wa Eshialhulo  fc kutoka  kata ndogo ya khaimba Franklin Mbati amesema vijana wake wako tayari kwa mapambano hayo na kuitaka serikali ya county kuhakikisha wachezaji  wanasaidia na vifaa vya matumizi.

Naye nahodha wa timu hiyo Ferdinand amesema watadumisha kiwango cha mazoezi na kuwataka wachezaji wenzake kuwa na nidhamu ya hali ya juu saana ili wasije wakaadhibiwa.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE