Vyongozi wa dini ya kiislamu Kanda ya Mumias Mashariki wamekuwa wa hivi punde kupinga uteuzi wa Martha Koome kama jaji mkuu jinsi ilivyopendekeza kamati ya kisheria nchini
Wakiongozwa na lmmam wa msikiti wa Jamia wa Makunga wilayani Mumias Mashariki vyongozi hao wanasema kuwa uteuzi huo haukuzingatia usawa wa kijinsia na hata kimaeneo
Wametaka nyadhifa muhimu kwenye idara mabimbali serikalini kuangazia maeneo yote ya nchi
Kuhusu swala la BBi Kiongozi huyo ametaka pawepo na naelewano kutoka pande zote kwenye swala nzima la katiba
Lubale amewatahadharisha vyongozi dhidi ya kuwalazimishia Wakenya katiba ambayo huwenda ukawa mzigo siku zijazo
Immam huyo amechukua fursa hiyo kuwatakia waislamu mfungo wenye heri akiwataka kudumisha umoja
By James Nadwa