Wito umetolewa kwa wahisani mbalimbali kujitokeza na kuwapa ufadhili wa masomo wanafunzi hasa kutoka eneobunge la Mlima Elgon walioandikisha matokeo bora kwenye mtihani wa kitaifa wa KCPE na ambao wanatoka katika familia zisizojiweza.

Mwenyekiti wa halmashauri ya shule ya msingi ya Chemondi S.A katika wadi ya Chesikaki eneobunge la Mlima Elgon John Kipsoboi anasema huenda wanafunzi wengi katika shule hiyo wakashindwa kujiunga na kidato cha kwanza iwapo  wahisani hawataingilia kati na kuwalipia karo.

Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Chemondi S.A Samson Litu Akoto akiwapongeza washikadau kutoka sekta mbalimbali kwa ushirikiano  uliopelekea mwanafunzi wa kwanza kujizolea alama mia nne na moja.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE