Shule mbambali zinazidi kusherehekea matokeo bora ya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane ambayo yalitangazwa wiki jana na waziri wa elimu profesa George Magoha huku ushirikiano wa washikadau mbalimbali ukichangia kuandikisha matokeo hayo bora.
Wazazi walimu na wanafunzi wa shule ya msingi ya Kimerin S.A kutoka wadi ya Chesikaki eneobunge la Mlima Elgon wamesherehekea matokeo ya kuridhisha ya mwaka huu ambapo mwanafunzi bora alijizolea alama mia nne na moja huku mwalimu mkuu wa shule hiyo Enos Sipanda akiwapongeza walimu wazazi na wananfunzi kwa ushirikiano mwema.
Aidha Sipanda amewasihi wahisani kuingilia kati na kusaidia kugharamia karo ya mwanafunzi huyo Venel Kibet ili kuafiki malengo yake baada ya kubainika kuwa anatoka katika familia isiyojiweza.
Kwa upande wake mwanafunzi bora Venel Kibet akiwa mwingi wa furaha na kudokeza kuwa ndoto yake ni kuwa muuguzi siku za usoni.