Wawakilishi wadi wa wanaoegemea mrengo wa chama cha ODM katika kaunti ya Kakamega wakiongozwa na kiongozi wa wengi katika bunge hilo Joel Ongoro, leo wamekuwa na mkao na kusisitiza kuwa gavana wa kaunti hiyo Wycliffe Oparanya hana mpango wa kuondoka chama cha ODM ili kufanya muungano na naibu wa rais William Ruto.

Wanasema kumekuwa na madai kuwa mkutano baina ya naibu wa rais William Ruto na gavana Oparanya ulikuwa wa kumshawishi kugura chama cha ODM na kufanya mkataba wa makubaliano ya kisiasa na Ruto.

 Wana ODM wanasema madai hayo ni njama ya wapinzani wa Oparanya katika eneo la magharibi waliongizwa kibaridi na usimamizi wa ODM ulikuwa unafahamu maandalizi ya mkutano huo

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE