Vyongozi kandhaa wanazidi kutoa hisia mseto kuhusu kudorora kwa elimu ya mtoto wa kiume siku moja tu baada ya kutolewa kwa matokeo ya mtiani wa darasa la nane nchini KCPE
Mwakilishiwadi wa Marama Central wilayani Butere Ondako Maina amesifia hali hiyo
Amehoji kuwa kwa muda mtoto wa kike amesalia nyuma haswa kimasomo na ni wakati wa juhudi zake kutambuliwa katika jamii
Kuhusu shule za Uma kufanya vema ikilinganishwa na zile za kibinafsi Ondako amesema kuwa huenda ilitokana na matayarisho duni kwa wanafunzi katika shule hizo za kibinafsi
Zaidi ya wanafunzi 500 wa shule za uma kutoka Wadi hiyo zikiwemo Bukolwe, Shitswitswi, Eshinamwenyuli , Ebulafu na ile ya Butere primary walipata alama 400 na zaidi huku Kiongozi huyo akiahidi kuwasaidia wasiojiweza kukamilisha masomo yao
By James Nadwa