Mwanamme mwenye umri wa miaka 26 amefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya nissan matatu kwenye barabara ya Kakamega-Webuye katika kituo cha kibiashara cha kambi mwanza.

Kulingana na waliyoshuhudia ajali hiyo wamehoji kuwa mwendazake aliyefahamika kama Francis Shikoli ambaye ni mfanyikazi  katika kichinjio cha kambi mwanza aligongwa na gari aina ya nissan matatu iliyokuwa ikiendeshwa kwa kasi ambapo ilimgonga alipokuwa akijaribu kuvuga barabara kuelekea upande wa pili.

Ni kisa kilichothibitishwa na naibu chifu wa kata ndogo ya Kakunga JustonAambulwa ambaye amewashauri wafanyibiashara wa eneo hilo pamoja na waendeshaji magari kuwa waangalivu wanapoendesha biashara yao katika eneo hilo.

By Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE