Wito umetolewa kwa wakaazi wa kaunti ya Bungoma kufwata kikamilifu mwongozo uliotolewa na serikali hivi maajuzi hasa agizo la marufuku ya kutotoka nje masaa ya usiku ili kuzuia msambao wa virusi vya corona.

Akihutubu kwenye hafla ya mazishi eneo la Chesikaki naibu chifu wa kata ndogo ya Chesikaki eneobunge la Mlima Elgon Mourice Wetala anasema ni wajibu wa kila mwananchi kuzingatia masharti hayo ikiwemo masaa ya kafyu na kutohudhuria ibaada ya jumapili ili kukabili msambao wa virusi vya corona.

Wakati uo huo Wetala amewahimiza wazazi kuwapa wanao mwelekeo ulio bora ili kuwaepusha kupotoka kimaadili  kando  kuwahimizwa kutumia stakabadhi zao wakati wanapowatafutia wanao vyeti vya kuzaliwa .

Naye afisa katika hazina ya CDF eneobunge la Mlima Elgon Robert Wasing’ong’o akidokeza kuwa tayari hazina hiyo imesambaza fedha za basari kwa baadhi ya shule eneo hilo.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE