Ziara yake Naibu wa Rais dakta William Ruto katika eneo bunge la Malava ambako alitarajiwa kuhudhuria ibaada katika kanisa la Holy Spirit lililoko eneo la Shivikhwa imehairishwa kufuatia kuwekwa kwa masharti zaidi ya kukabili covid 19 katika kaunti ya Kakamega.

Wakiwahutubia wanahabari kwenye makao makuu ya kanisa hilo mjini Malava, viongozi wanaoegemea upande wake Naibu wa Rais wakiongozwa na aliyekuwa seneta wa Kakamega Bony Khalwale wamesema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo ili kuisaidia serikali katika juhudi za kupigana na covid 19.

Hata hivyo wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta kueka mikakati kabambe ya  kupigana na janga hilo huku wakiwataka maafisa wa polisi kutotumia fursa hiyo kuwahangaisha wananchi.

Shem Shamalla ni askofu mkuu wa kanisa hilo nchini ambaye amewataka wananchi kuwa watulivu na kuendelea kufuata masharti hayo ya wizara ya afya katika kukabili Gojwa la covid 19. 

by Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE