Bawabu mmoja anayelinda maduka mjini Kakamega amepata majeraha mabaya na kuwachwa hali maututi baada ya kupigwa na kukatwakatwa na majambazi alfajiri ya leo  baada ya muda wa kafyu.

Kulingana na walioshuhudia kisa hicho wakiongozwa na Wycliffe Okumu mmoja wa walinzi hao wa usiku wanasema kuwa majambazi wakiwemo watoto wa kurandaranda wamekuwa  wakiwashambulia na hata kuwaua baada ya muda wa kafyu kutamatika.

Wanasema kuwa visa vya walinzi hao wa usiku na wenyeji kushambuliwa na  kuwaua vimeongezeka mjini humo haswa masaa ya alfajiri huku wakinyoshea kidole cha lawama idara ya polisi kuzembea kazini huku wakitaka polisi kufanya doria hata baada ya muda wa kafyu kutamatika kuzuia uhalifu huo.

By Linda Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE