Serikali kupitia wizara ya elimu imetaakiwa kuzifadhili shule kifedha ili kuhakikisha wanafunzi wakiwemo watakaojiunga na kidato cha kwanza mwezi ujao wanapata elimu bila wasiwasi

Haya ni kulingana na mwenyekiti wa wanaume wakatoliki CMA jimbo la Kakamega Vitalis Arunga ambaye amesema wazazi wengi wanapitia hali ngumu kiuchumi wakati huu wa janga la corona, jambo linaloathiri masomo ya watoto wao.

Arunga hata hivyo amewataka wazazi kujikaza kuwalipia wanao karo licha ya hali ngumu wanayopitia huku akiwataka kuelewana na wasimamizi wa shule kuhakikisha wanao wanapata elimu itakayo wasaidia kimaisha.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE