Wakaazi wa kata ya Chesikaki eneobunge la Mlima Elgon wamehimizwa kufwata kanuni za ununuzi wa ardhi ili kusitisha visa vya malumbano kati ya wauzaji na wanunuzi ambavyo vimekuwa  vikishuhudiwa miongoni mwa baadhi ya wenyeji eneo hilo.

Akihutubu kwenye hafla ya mazishi ya Davis Watima eneo la Chesikaki naibu chifu wa kata ndogo ya Chesikaki Mourice Wetala amewataka wakaazi, kuhakikisha wananunua kipande cha ardhi ambacho kina cheti cha umiliki ili kuzuia migogoro ambayo imekuwa ikishuhudiwa kwa baadhi ya wakaazi.

Wakati uo huo Wetala amewasihi wazazi kushirikiana kikamilifu na bodi za shule iwapo wanatarajia matokeo ya mitihani ya kitaifa kuimarika katika shule za eneo hilo.

Ni semi zilizotiliwa mkazo na naibu chifu wa kata ndogo ya chemondi martin naibei.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE