Serikali imetakiwa kufanya matibabu ya saratini kuwa ya bure katika hospitali zote nchini kuepusha maafa yanayotokana na ukosefu wa hela za kumdu gharama ya matibabu hayo

Ni wito wake shirika lisilo la kiserikali la tuinuane lililoko kaunti ya Kakamega baada ya kuongoza mchango wa kusaidia matibabu ya saratani ya macho kwa mtoto wa mshirika wao Micheal na mama Abigael Akatuu katika eneo la Ematsayi Bukara Kakamega ya kati,, Evans Shimonyo ni mshirikishi wa shirika hilo.

 Ni swala ambalo limeungwa mkono na mshirikishi mkuu wa kaunti ya Kakamega David Imamba ambaye ametaka uchunguzi wa saratani kufanywa katika hospitali zote nchini ikiwemo zile za zahanati.

Wazazi wa mtoto mwenye umri wa miaka minne ambaye ameathrika na saratani hiyo ya macho zote wamesema kuwa gharama ya juu ya matibabu ya ugonjwa huu imewamaliza bila kuona mabadiliko na sasa wanaomba yeyote kuwasaidia kugharamia matibabu hayo katika hospitali ya Kenyatta. 

Nao wanachama wa shirika hilo wakiongozwa na Harrison  Wesa Khachina wamesifia ushirikiano ambao wanachama hao wako nao kusaidia wenzao wakati wa shida na kuitaka serikali kuwapiga jeki kwa kuwapa mikopo midogo ya kuwawezesha kuinua biashara zao.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE