Hatua ya kujiondoa kwake mbunge wa Malava Malulu Injendi kutoka chama cha Jubilee na kujiunga na chama cha ANC imezidi kukashfiwa vikali na baadhi ya viongozi na wakaazi wanaoegemea upande wake naibu wa Rais dakta Wiliam Ruto kutoka eneo hilo wakiitaja kuwa isiyo na msingi wowote
Wakiongozwa naye Kevin Mahelo ambaye ni mwakilishi wa wadi ya Butali Chegulo, wanasema kwamba kujiondoa kwake Malulu kutoka chamani humo hakutatikisa kwa vyovyote vile umaarufu wake naibu wa rais eneo hilo wakishinikiza kuwa wataendelea kumuunga mkono katika azma yake ya kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2022
Kauli sawia ikitolewa na baadhi ya wakaazi kutoka eneo bunge la Malava ambao wameelezea kusikitishwa kwao na hatua yake Malulu Injendi ambaye alikuwa mwandani wa karibu wa naibu wa Rais ya kugura chama cha Jubilee licha ya mingi ya miradi ya maendeleo ambayo dakta William Ruto ameweza kutekeleza katika eneo bunge lake.
By Richard Milimu