Siku chache baada ya wakazi wa Butere kulalamikia kuzorota kwa usalama, sasa wamepongeza mipangilio ya idara ya usalama kukabili visa vya uhalifu
Wakiongozwa na Habil Nanjendo baada ya kukutana na baadhi ya wakuu wa usalama, wakazi hao kupitia kwa mwanasiasa Habil Nanjendo wamesema wana matumani ya usalama kuimarika
Nanjendo amehimiza maafisa wa usalama kushirikiana na wananchi na kuunda urafiki ili kupata ripoti za kuimarisha usalama