LUBAO FREQUENCY MODULATION LIMITED

Uniting Communities
  1. Listen to Lubao FM Live 102.2 FM

Live now:

Up next:

Wakenya wazidi kuonyesha maoni yao kuhusu swala la fedha la imf (international monetary fund)

Chini ya alama ya reli #stoploaningkenyawakenya wanaendelea kuelekeza hasira zao katika kurasa za mitandao ya IMF, chini ya alama ya reli #stoploaningkenya wakisisitiza mkopo huo utayafanya maisha kuwa magumu zaidi hasa kipindi hiki taifa linapoendelea kung’atwa na makali ya janga la covid-19.

Hii ni baada ya serikali kuomba mkopo huo na ambao umeidhinishwa, ikihoji utasaidia kuimarisha kampeni dhidi ya virusi vya corona nchini.

Wakenya  bado wameshikilia kuwa mkopo huo utaishia mifukoni mwa mafisadi  huku wakihimiza shirika hilo kufuta mkopo huo katika kila chapisho la IMF mitandaoni.

Mkopo wa sh257 bilioni uliopewa serikali ya Kenya wiki jana na shirika hilo la fedha duniani (IMF) ukipingwa na wakenya ambao wamekasirishwa na ukopaji wa kila mara hamaki za wakenya zinaendelea kushuhudiwa mitandaoni, serikali nayo ikianza msako kuzima wanaoikosoa facebook na twitter.

By Austin Shambetsa

Charles Oduor

Read Previous

Paris St Germain wafanya mawasiliano na wawakilishi wa mshambuliaji nyota wa liverpool Mohamed Salah

Read Next

Wanabodaboda Kaunti ya Bungoma kulalamikia Hali ngumu ya maisha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *